Mfumo kamili wa POS, Inventory, Ripoti za Fedha, na Akili ya Biashara — yote kwenye simu yako.
Zana zote za kisasa kwa biashara yako — bila matatizo
Fanya mauzo haraka, pokea malipo ya cash, M-Pesa, au credit. Risiti moja kwa moja.
Fuatilia stock kwa wakati halisi. Onyo la kuisha stock, dead stock, na mapendekezo ya reorder.
Faida, hasara, matumizi, na mauzo — kwa siku, wiki, mwezi, na mwaka. Graphs nzuri.
ABC Classification, KPI Dashboard, Profit Ranking, na Inventory Health Score.
Cashier, Staff, Manager — kila mmoja ana uwezo wake. Login tofauti, data salama.
Inafanya kazi vizuri kwenye simu, tablet, na kompyuta. Bila app ya kudownload.
Mtandao ukikatika, endelea kuuza. Mauzo yanahifadhiwa kwenye simu na kutumwa mtandao ukirudi, app ikiwa wazi.
Scan bidhaa kuuza haraka, chapisha lebo za barcode, na pokea malipo kwa QR — mteja anaskani na kulipa mwenyewe.
Jikoni, IMEI/serial, Expiry na Size/Rangi huonekana kwa aina za biashara zinazozihitaji tu. Duka la vifaa haliangalii jikoni, mgahawa hauangalii IMEI.
Fuatilia simu kwa IMEI au serial, tarehe ya kuisha kwa bidhaa, na bidhaa zenye size au rangi tofauti.
Kwa migahawa, juice na bakery: orodha ya vyakula, recipe, na oda zinazoenda jikoni.
Pokea M-Pesa, Mixx by Yas na benki. ClickPesa inathibitisha malipo moja kwa moja (Premier, kwa ombi).
Uza kwa mkopo kwa wateja, fuatilia wanaodaiwa, na madeni ya wasambazaji.
Tengeneza Purchase Orders na ufuatilie wasambazaji wako (Biashara na Premier).
Simamia maeneo au matawi yako yote kutoka akaunti moja. Biashara maeneo 3, Premier bila mipaka.
Jua nani alifanya nini na lini. Hatua muhimu za watumiaji zinarekodiwa (Premier).
Uliza swali kwa lugha ya kawaida kuhusu mauzo na stock yako na upate jibu papo hapo (Premier).
Kuanzia leo hadi unauza — bila ugumu.
Jaza fomu fupi, chagua kifurushi. Tunawasiliana nawe ndani ya masaa 24, na miezi 3 za kwanza ni bure — bila kadi ya benki.
Ongeza bidhaa zako (moja moja au kwa CSV), weka bei, na waongeze wafanyakazi — kila mmoja na nafasi yake.
Tumia POS kwenye simu yako. Ripoti, faida na ushauri wa stock vinatokea vyenyewe kadri unavyouza.
Hakuna kuandika namba kwa mkono, hakuna "nimetuma, hujaona?". Bili moja, QR moja — na pesa zinaingia kwenye akaunti yako.
Weka bidhaa kwenye kikapu cha POS. Punguzo, bei ya jumla na huduma vyote vinahesabiwa kama kawaida.
Mfumo unatengeneza bili yenye namba yake na QR code. Kikapu kinafutwa, kwa hiyo unaweza kumhudumia mteja anayefuata mara moja.
Anafungua bili kwenye simu yake — bila kupakua app wala kuingia. Anaona bidhaa, jumla, na namba za kulipia ulizoweka: M-Pesa Lipa Namba, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki.
Analipa kutoka kwenye simu yake, na pesa zinaingia kwenye akaunti yako mwenyewe — hakuna mtu wa kati.
Ukiona SMS ya pesa kwenye simu yako, chagua njia ya malipo na weka namba ya muamala, kisha bonyeza Thibitisha. Mauzo yanarekodiwa, stock inapungua, na risiti kamili inatoka.
Mteja hawezi kutumia SMS moja kulipia bili mbili. Mfumo unakataa namba iliyokwisha tumika.
Kila bili ina muda wake. Unaweza kuonyesha QR tena, kuthibitisha, kuchapisha au kughairi — bila kupoteza mteja mwingine.
Chapisha bili ndogo yenye QR ya mteja kuchukua. Imeandikwa "BILI (si risiti)"; risiti kamili inatolewa baada ya malipo.
Meneja anaweka namba za kupokelea malipo mara moja. Kila bili inazionyesha kwa mteja kiotomatiki.
Picha halisi kutoka kwenye mfumo — si michoro.
POS: chagua bidhaa, kikapu kinajijaza, na unapokea malipo ya cash, M-Pesa au mkopo kwa mibofyo michache.
Mfumo hauhifadhi data tu — unakuambia cha kufanya: nini cha kuagiza, nini hakiuzi, na wapi faida inatoka.
Mapato, faida, margin na matumizi kwa siku 7, 30 au 90 — pamoja na ulinganisho na kipindi kilichopita.
Bidhaa zipi zinakuletea faida zaidi, na zipi zinauzika lakini faida ni ndogo.
Bidhaa zisizouzika kwa siku unazochagua, thamani ya pesa iliyokwama, na pendekezo la cha kufanya.
Orodha ya bidhaa za kuagiza na kiasi, kulingana na jinsi zinavyouzwa.
Alama moja inayoonyesha afya ya stock yako, na vitu vinavyoihusu: stock ndogo, stock nyingi, na dead stock.
Mauzo, gharama, matumizi na faida halisi kwa kipindi chochote, tayari kuonyesha benki au mwenzako.
Mtandao wa Maduka unaunganisha matawi yako yote — uone biashara nzima kwa mara moja, huku kila tawi likiendelea na data yake.
Mauzo, faida ghafi, matumizi na faida halisi ya kila tawi na jumla yake, kwenye ukurasa mmoja.
Fanya kazi kwenye tawi lolote la mtandao wako bila kutoka na kuingia upya.
Kila tawi lina bidhaa, mauzo na wafanyakazi wake. Wafanyakazi wa tawi wanaona tawi lao tu; mmiliki ndiye anayeona mtandao mzima.
Hukupata jibu? Tuandikie WhatsApp, tunajibu haraka.
Hapana. Simu yako inatosha. Inafanya kazi pia kwenye tablet na kompyuta, na unaweza kuiweka kwenye home screen kama app ya kawaida bila kupitia App Store.
Ndiyo. Mauzo ya kawaida yanahifadhiwa kwenye simu na kutumwa mtandao ukirudi, app ikiwa wazi. Baadhi ya vitu vinahitaji mtandao: mauzo ya mkopo, malipo ya ClickPesa, IMEI na jikoni.
Ndiyo. Wateja wapya wanapata miezi 3 za kwanza bila malipo na bila kadi ya benki. Ofa hii ni ya mara moja tu unapoanza, na unaweza kuacha wakati wowote bila adhabu.
Unalipa kwa siku unazotaka kulipia — hakuna setup fee. Kwenye sehemu ya Bei andika idadi ya siku uone gharama kamili na tarehe zinapoishia.
Kila duka lina data yake, tofauti na maduka mengine — unaona tu data ya duka lako. Wafanyakazi wanaona kulingana na nafasi zao: cashier hawezi kubadilisha bei wala kuona ripoti za fedha.
Ndiyo. Kila mfanyakazi ana login yake na nafasi yake (Cashier, Staff, Manager). Idadi ya watumiaji na maeneo inategemea kifurushi — angalia sehemu ya Bei.
Kwenye fomu ya usajili chagua "Kampuni yenye matawi". Tutakufungulia mtandao mmoja wenye matawi yako yote: unaona muhtasari wa mauzo, faida na matumizi ya kila tawi, na unabadilisha tawi kwa bonyeza moja. Kila tawi linaendelea na data yake. Bei ni maalum kulingana na idadi ya matawi — tuandikie WhatsApp.
Unaweza kuongeza bidhaa moja moja, au kuingiza nyingi kwa mara moja kwa faili la CSV. Ukihitaji msaada wa kuhamisha data zako za zamani, tuandikie WhatsApp.
Unabonyeza "Lipa kwa QR" kwenye POS, na mfumo unatengeneza bili yenye QR. Mteja anaskani kwa kamera ya simu yake (bila kupakua app wala kuingia), anaona bili na namba za kulipia, kisha analipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki. Pesa zinaingia kwenye akaunti yako.
Wewe unathibitisha baada ya kuona pesa kwenye simu au akaunti yako: unachagua njia ya malipo na kuweka namba ya muamala, kisha mauzo yanarekodiwa na risiti inatoka. Namba ya muamala haiwezi kutumika mara mbili. Uthibitisho wa moja kwa moja upo kwa ClickPesa (kifurushi cha Premier, kwa ombi).
Tupo WhatsApp na simu: +255 768 139 301. Tunatoa support na updates za mfumo bure.
Duka Langu inafanya kazi kama app ya kawaida — haraka, rahisi, na mauzo ya kawaida yanaendelea hata mtandao ukikatika. Hakuna haja ya kudownload kutoka App Store.
Mfumo una ngazi 4 za uwezo — kila mfanyakazi anaona sehemu yake tu
Mfanyakazi wa mstari wa mbele — anafanya mauzo haraka na kwa usalama. Hana uwezo wa kubadilisha bei au kuona ripoti za fedha.
Mfanyakazi wa kawaida — ana uwezo zaidi ya cashier. Anaweza kuona ripoti za msingi na kusaidia na inventory.
Msimamizi wa duka — ana uwezo karibu wote. Anaweza kusimamia wafanyakazi, kuona ripoti zote, na kubadilisha mipangilio mingi.
Msimamizi mkuu wa mfumo — ana uwezo wa usimamizi wa kiwango cha juu. Anashughulikia uendeshaji wa kiufundi na ufuatiliaji wa mfumo wote.
Kila duka lina data yake — salama na tofauti na maduka mengine. Unaona tu data ya duka lako.
Miezi 3 bure ya kuanza kwa wateja wapya — hakuna kadi ya benki.
Miezi 3 za kwanza ni bure (mara moja tu). Baada ya hapo unalipa kwa siku unazotaka kulipia.
Kwa duka dogo linaloanza
Usimamizi kamili wa duka
Udhibiti kamili bila kikwazo
Kwa wenye maduka mengi
Chagua kifurushi na utumie vipengele vyake vyote bure kwa miezi 3 za kwanza. Ofa hii ni ya mara moja tu unapoanza — haijirudii kila mwaka. Hakuna kadi ya benki, na unaacha lini unataka bila adhabu.
Jaza fomu — tutawasiliana nawe ndani ya masaa 24 kupitia WhatsApp au Email na kukusaidia kuanza.
Jaza fomu hii — tutawasiliana nawe ndani ya masaa 24